Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Mohamed Kimweri (kushoto),
akizungumza katika na wandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu
kampuni hiyo kupata haki za kuonesha michuano ya Copa Amerika moja kwa
moja ambayoitafanyika nchini Marekani kuanzia Juni 3 mpaka Juni 26 mwaka
huu. Kulia ni Meneja Maudhui wa kampuni hiyo, Paulina Kimweri.
Meneja Maudhui wa kampuni hiyo, Paulina Kimweri, akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya StarTimes
Tanzania imefanikiwa kupata haki za kuonyesha michuano ya Copa America
moja kwa moja ambayo itafanyika nchini Marekani kuanzia Juni 3 mpaka
Juni 26 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi
wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi huo Makamu wa
Rais wa kampuni hiyo nchini, Zuhura Hanif alisema kuwa kupatikana kwa
haki za kuonyesha michuano hiyo mikubwa na mikongwe ulimwenguni ikiwa
inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake ni jitihada za kuhakikisha
kuwa wateja wao wanafurahia vipindi bora vya michezo na burudani.
“Leo StarTimes inayo
habari njema kuwataarifu kuwa tumepata haki maalum za kuonyesha michuano
ya Copa America moja kwa moja kutoka nchini Marekani kuanzia Juni 3
mpaka Juni 26 mwaka huu. Ninaposema haki maalumu manake ni kwamba
watanzania hawataweza kushuhudia michuano hii sehemu yoyote isipokuwa
kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee.
Alisema wateja wao na
wapenzi wa soka nchini wataweza kushuhudia michezo yote 32 ambapo
itazikutanisha timu 16 za bara la Amerika ya Kusini na mwenyeji Marekani
zitazoumana katika viwanja 10 tofauti nchini Marekani ikiwa ni kwa mara
ya kwanza kufanyikia huko.” Alisema Hanif.
Hanif aliwataka
watanzania na wapenda soka kwa ujumla kujiandaa kushuhudia mechi kali za
miamba ya soka kutoka bara la Amerika ya Kusini ambazo itayakutanisha
majina makubwa katika ulimwengu wa mpira wa miguu kama vile; Lionel
Messi, Kun Aguero (Argentina), Alexis Sanchez, Arturo Vidal (Chile),
Neymar, Marcelo (Brazil), Luis Suarez, Edinson Cavani (Uruguay) na
wengineo.
“Ninafahamu kuwa
watanzania ni miongini mwa mashabiki wakubwa wa mchezo wa soka hivyo
watafurahia zaidi kuwatazama wachezaji wanaowapenda wakiwakilisha
mataifa yao katika michuano hii. Tayari tumekishashuhudia ligi
mbalimbali ulimwenguni zikielekea ukingoni kama vile ligi za Bundesliga
na Serie A za Ujerumani na Italia ambazo tayari timu za Bayern Munich na
Juventus zimaeshatangazwa mabingwa. Na nafurahi kuwa ligi hizo zote
mbili zilionekana moja kwa moja kwenye chaneli za michezo za ving’amuzi
vyetu kwa malipo ya gharama nafuu kabisa ya mwisho wa mwezi kuanzia sh.
5,000 aliongezea
“Ningependa kuchukua
fursa hii kuwataka watanzania na wateja wetu kwa ujumla kuwa michezo na
burudani kwetu StarTimes ndio nyumbani. Kwa kuliona hilo baada ya
kufaidi mechi za ligi kuu za Ujerumani na Italia sasa tumewaletea Copa
America kuhakikisha kuwa mnafurahia vema luninga zenu.
Mbali na michuano hii
tunaahidi kuendelea kuwaletea michuano mingine kama awali tulivyofanya
kwa Kombe la Dunia la Wanawake, Kombe la Vilabu Bingwa Duniani, Kombe la
Dunia la Vijana chini ya Miaka 20 na miningineyo. Nawasihi wateja wetu
kukaa mkao wa kula na wasiojiunga nasi wafanye hivyo ili kufaidi uhondo
huu utakaowajia hivi punde kwenye luninga zao.” Alisema Hanif.
Michuano ya Copa Amerika
inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Juni kuanzia tarehe 3 mpaka 26
mwaka 2016 ni michuano mikongwe zaidi duniani ikiwa inatimiza miaka 100
tangu kuanzishwa kwake ambapo nchi ya Uruguay inashikilia rekodi ya
kuchukua mara nyingi zaidi, mara 15 ikifuatiwa na Argentina mara 14.
Michuano ya mwaka huu itakuwa ni ya kusisimua zaidi hasa kwa bingwa
mtetezi nchi ya Chile kutetea ubingwa wake, ambapo aliuchukua mwaka 2015
baada ya kuishinda timu ya taifa ya Argentina kwa mikwaju ya penati.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment