Mmiliki
wa Leicester City ambaye pia ni mfanya biashara kutoka Thailand, Vichai
Srivaddhanaprabha amewapa wachezaji 30 wa kikosi cha Leicester City
gari aina ya Mercedes B-Class zilizo na thamani ya Pauni 32,670 sawa na
Milioni 103 za kitanzania kila mmoja ikiwa ni zawadi ya kutwaa ubingwa
la Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza.
Wachezaji wa Leicester City wakishangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Sportsmail umeeleza kuwa baada ya
Srivaddhanaprabha kutoa zawadi hiyo, itamgharimu kiasi cha Pauni Milioni
moja kuwanunulia wachezaji wote 30 aina hiyo ya magari.
Aidha
tayari bilionea huyo ameshakiahidi kikosi cha Claudio Ranieri kuwa
atagharamia gharama za kuwapeleka Las Vegas ikiwa ni sehemu ya
kusherekea mafanikio waliyopata msimu wa 2015/2016.
No comments:
Post a Comment