VAN GAAL ADAI KUTWAA KOMBE NI MUHIMU KULIKO KUCHEZA ULAYA
Jumamosi Man United watacheza Fainali ya FA CUP Uwanjani Wembley dhidi ya Crystal Palace wakiwania kulitwaa Kombe hilo kongwe Duniani kwa mara ya kwanza tangu 2004.
Wengi
wa Wachambuzi hao wanaamini kuwa mara baada ya FA CUP Man United
itamtimua Van Gaal aliebakisha Mwaka Mmoja kwenye Mkataba wake na
kumchukua Jose Mourinho. Lakini mwenyewe Van Gaal anaona kubeba FA CUP ni muhimu kupita kucheza UCL kwani inaleta Kombe Klabuni.
Van
Gaal ameeleza: “Kufuzu Ulaya si Taji…Taji ni FA CUP, ni Ubingwa. Ni
muhimu kwa Wachezaji. Watabeba Kombe na kukumbuka hasa kwa hapa England
kwani FA CUP ni Taji kubwa!”
DONDOO MUHIMU: -Hii ni Mechi ya Fainali ya 135 ya FA CUP.
-Fainali hii ni kama Marudio ya Fainali ya Mwaka 1990 ambayo Manchester United waliifunga Crystal Palace 1-0 baada ya Mechi ya kwanza kwisha Sare 3-3.
-Hii ni mara ya Pili kwa Palace kutinga Fainali wakati kwa Man United ni Fainali ya 18 na wameshinda 11 kati ya hizo wakipitwa tu na Arsenal walioshinda Fainali 12
-Mara ya mwisho kwa Man United kutwaa FA CUP ni Mwaka 2004 walipoifunga Timu ya Daraja la Kwanza Millwall 3-0. Van Gaal atatinga kwenye Fainali hiyo akiwa na Kikosi kamili ukimwondoa Luke Shaw ambae bado hajawa fiti licha ya kuanza tena Mazoezi baada ya kuvunjika Mguu mara mbili Mwezi Septemba.
Pia Kungo Marouane Fellaini sasa yuko huru kucheza baada ya kumaliza Kifungo chake cha Mechi 3.

FA CUP
Fainali
Jumamosi Mei 21
Saa 1:30 usiku
Uwanja wa Wembley, London
Manchester United v Crystal Palace
Post a Comment