KIPA Denis Richard Dioniz wa Geita
Gold ameshinda rufaa yake aliyowasilisha Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huku rufaa zingine saba zikitupiliwa mbali.
Akizungumza na wandishi wa habari
leo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya rufaa ya nidhamu Wakili Revocutus Kuhuli alisema
kamati yake ilipokea rufani nane za
viongozi, mchezaji na timu tatu zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania
Bara 2015/2016 lakini kipa Denis pekee aliyeshinda
Uamuzi huo wa Kamati umetangazwa
uamuzi huo mbele ya wandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi za
TFF, zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es
Salaam.
Jumla ya rufaa nane zinazohusu timu,
kocha, viongozi na mchezaji mmoja zilijadilikuwa na kamati hiyo Mei mosi, 2016
kwenye ofisi za TFF jijini.
Rufaa zilizojadiliwa kwenye kikao
hicho ni za Timu ya Geita Gold, Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya
soka ya Geita Gold FC, Denis Richard Dioniz - Kipa wa Geita Gold, Fatel
Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora
Wengine Salehe Mang’ola – Mwamuzi wa
Soka wa Mkoa wa Dodoma, Timu ya Soka ya Polisi Tabora, JKT Oljoro Fc ya Arusha
na Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora
Wadau hao wa soka walikata rufaa
dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia hatiani na
kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza.
Pia Wakili Revocutus alisema kama
warufani hawataridhika na hukumu hiyo wanaweza kukataa rufaa ndani ya siku
kumi.
No comments:
Post a Comment