CLAUDIO RANIERI MENEJA BORA ENGLAND
Ranieri, Raia wa Italy mwenye Miaka 64, amezoa Tuzo hiyo iliyotolewa na LMA, League Managers' Association, Chama cha Mamenej wa Ligi huko England, kwa kuiongoza Leicester kutwaa Ubingwa wao wa kwanza katika Histiria ya Klabu yao ya Miaka 132.
Mbali ya Tuzo hiyo, Pia Ranieri alipewa Tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka kwa Ligi Kuu England ambapo MTuzo nyingine zilikwenda za Mameneja wa Madaraja tofauti zilikwenda kwa Chris Hughton wa Brighton alitwaa ile ya Daraja la Championship, Gary Caldwell wa Wigan alitwaa ya Ligi 1 na Chris Wilder wa Northampton kutwaa ya Ligi 2.
Msimu huu, Ranieri alizoa Tuzo za Meneja Bora wa Ligi Kuu England mara 3 na huko kwao Italy pia ametunukiwa kuwa ndie Meneja Bora wa Mwaka.
Brighton walimaliza Nafasi ya Tatu kwenye Ligi ya Daraja la Pili, Championship, na Jana walitupwa nje ya Mchujo wa kusaka Timu ya Tatu kuungana na Burnley na Middlesbrough kupanda Daraja kuingia Ligi Kuu England baada ya kutolewa na Sheffield Wednesday
Post a Comment