Mfilipino huyo ambaye alishindwa katika pigano lake kuu dhidi ya bondia tajiri zaidi duniani Floyd Mayweather amekuwa bingwa katika vitengo mbali mbali katika kipindi cha miaka 21 iliyopita tangu alipoanza ndondi.
Pacquiao alishinda kwa wingi wa pointi katika pigano hilo lililokuwa likitazamiwa na wengi. Pacquiao, amekuwa mbunge tangu mwaka wa 2010.
Amesema kuwa anastaafu ndondi za kulipwa iliawahudumie wananchi kisiasa.
Mfilipino huyo mcha mungu na muaniaji kiti cha useneta nchini kwao alithibitisha udedea wake ulingoni alipomuadhibu vikali mmarekani huyo.
No comments:
Post a Comment