LUKE SHAW KUREJEA MAZOEZINI MWEZI UJAO
Shaw, mwenye Miaka 20, aliumia huko Amsterdam, Netherlands hapo Septemba 15 katika Mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI ambayo Man United walifungwa 2-1 na PSV Eindhoven kufuatia kukatwa na Beki Hector Moreno.
Ikiwa Shaw atarejea vizuri Mazoezini Mwezi Aprili basi anaweza kupata Mechi kabla Msimu huu wa 2015/16 kumalizika katikati ya Mwezi Mei.
Kukosekana
kwa Luke Shaw kwenye Kikosi cha Man United Msimu huu kulimlazimisha
Meneja Louis van Gaal kutumia Makinda wa Chuo cha Soka chao kina Joe
Riley, Timothy Fosu-Mensah na Cameron Borthwick-Jackson kwenye Nafasi ya
Fulbeki wa Kushoto ambayo pia Winga Ashley Young alichezeshwa.
Post a Comment