NDANI
ya Siku 3, Kinda wa Miaka 18, Marcus Rashford, ameibuka na kupiga Bao 4
katika Mechi zake 2 za kwanza kabisa akiichezea Manchester United, na
kuibua gumzo kubwa huko England na kila kona ya Dunia. Majuzi
Alhamisi, Marcus Rashford, akichezea Kikosi cha Kwanza cha Man United
kwa mara ya kwanza, alipoingizwa bila kutarajiwa kabla ya Mechi kuanza
baada ya kuumia Anthony Martial wakati akipasha moto, alipiga Bao 2
wakati Man United inaitwanga FC Midtjylland 5-1 katika Mechi ya UEFA
EUROPA LIGI. Na Jumapili, ndani ya Old Trafford, Marcus Rashford,
alipiga Bao 2 tena na kuweka Rekodi ya kuwa Kijana mdogo kabisa katika
Historia ya Man United kufunga Bao za Ligi wakati Man United inawabonda
Arsenal 3-2 Uwanjani Old Trafford. Mbali
ya Siku hii kuwa ya Marcus Rashford, Wadau wengi sasa wameanza kukata
tamaa kwa Arsenal kutwaa Ubingwa Msimu huu hasa baada ya kujikuta sasa
wako palepale Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Tottenham, walio
Nafasi ya Pili, na Pointi 5 nyuma ya Vinara Leicester City. Lakini
kilichowaumiza wengi, hasa Wadau wa Arsenal, ni kufungwa na Kikosi
dhaifu cha Man United ambacho kilikosa karibu Robo 3 ya Wachezaji wao wa
kawaida na kuwatumia Makinda ambao kila Mtu alitegemea watafagiwa na
Masupastaa wa Arsenal kina Mesut Ozil, Alexis Sanchez, Aaron Ramsey na
kadhalika.
NINI WAMESEMA BAADA YA KIPONDO HIKI: Arsene Wenger kwa Arsenal: "Tulitanguliwa
kufungwa nah ii ilileta ugumu. Kinachosikitisha tulimiliki sana Mpira
na kuruhusu Bao 3. Tumepoteza Pointi 3 muhimu hii Leo na inabidi
tushinde Jumatano.” Alipohojiwa kama kipigo hiki kitaathiri nafasi yao ya kutwaa Ubingwa, Wenger alijibu: “Hakuna anaejua!” Kuhusu
Marcus Rashford, Wenger, akikiri kutomjua, alisema: “Alinishangaza kwa
mwendo wake golini na akili zake. Huyu ataishangaza Man United!”
Lejendari wa Arsenal Thierry Henry: "Sidhani
hili lingetokea enzi zote wakati nacheza. Huu si uchezaji wa Timu
inayosaka Ubingwa. Hili ndio kama shabiki wa Arsenal nalitazama lakini
sina hakika Timu hii inaweza kuwa Bingwa. Hakuonyesha! Lakini bado wamo
mbio za Ubingwa lakini Leo walikuwa wa pili kwa kila kitu!” Akimgeukia
Rashford, Henry alisema: “Mbali ya kufunga Goli 4 Mechi 2, uchezaji
wake na jinsi anavyopenya kwenye nafasi, kumiliki na kuhodhi mpira,
kunaonyesha ana dhamira kubwa. Anajua nini kinaendelea, ametulia kwenye
Boksi, vile Vichwa na pia anafanya zile kazi ngumu na chafu Uwanjani!”
Louis van Gaal: "Nasikia
fahari kubwa, nimeridhika na nina furaha kwa sababu tulifanya na
Shrewsbury, tumefanya na Midtjylland na sasa tumefanya dhidi ya Timu
nzuri sana ya Ligi Kuu England, nimefurahishwa!” Juu ya Marcus Rashford, Van Gaal alisema: “Alicheza vizuri na ile Timu ya Denmark lakini na Arsenal amecheza vizuro mno!”
Marcus Rashford: "Ilikuwa Gemu yangu ya kwanza kwenye Ligi na ni ajabu. Kupiga Bao 2 ni bonasi!"
JAFO AANZA KUTEKELEZA AHADI ZAKE KISARAWE
-
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza katika kikao
cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kuwashukuru wajumbe
mara...
Serengeti: Untamed.
-
VAST. RELENTLESS. ALIVE.
Forget everything you know about time.
Witness the relentless thunder of the Great Migration. Track the ancient
...
Michezo : New King Imeichapa Malindi Bao 2-1
-
Mchezaji wa Timu ya Malindi akimiliki mpira akijiandaa kumpita beki wa Timu
ya New King, katika mchezo wa Ligi Kuu ya PBZ Zanzibar 2-25 /2026 mchezo
uliyo...
Post a Comment