Na Rahel Pallangyo
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wamiliki
na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu
walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.
Katika taarifa ambayo imetolewa na Katibu Mkuu wa Basata, Geoffrey Mwingereza ni marufuku kukusanya watoto katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ katika msimu huu wa Sikukuu ya Pasaka ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.

Pia wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na
vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda wa utumizi wa kumbi,
kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na
kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao.
Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kuendekeza faida katika biashara zao kiasi cha kuandaa madisko ya watoto hali mbayo imekuwa ikisababisha maafa ambayo yangeepukika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.
Aidha, baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa kumbi kwa msingi huohuo wa kuendekeza faida pasi na kujali maelekezo ya vibali vyao wamekuwa wakijaza watu kupita viwango vya madaraja waliyopangiwa na BASATA.
BASATA kama mtoaji wa vibali vya kumbi za sherehe na burudani linasisistiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote utakaokiuka maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya.
BASATA linawatakia wasanii na wadau wote wa Sanaa Pasaka njema na yenye furaha tele.
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

No comments:
Post a Comment