Hii inafuatia kauli ya chipukizi huyo ya timu ya taifa ya Uingereza na badala yake kujiunga na vigogo wa soka ya Afrika Super Eagles ya Nigeria.
Iwobi ameshajumuishwa katika kikosi cha Nigeria kinachoratibiwa kuchuana dhidi ya Misri siku ya Ijumaa 26 -29 Machi katika mechi ya kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika.
England imeanza harakati za kumshawishi asijiunge na Nigeria kwani hilo litawanyima fursa ya kumshirikisha katika timu ya taifa ya England.
Jarida la Daily Mirror linaripoti kuwa harakati za kimya kimya zinafanywa ilikumshawishi Iwobi abadilishe kauli yake kabla ya Ijumaa, kwani akishaichezea Super Eagles itakuwa vigumu mno kuichezea England katika mechi za kimataifa.
No comments:
Post a Comment