Lakini Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anategemea Kipa wake Petr Cech ataendeleza rekodi yake ya kutowahi kufungwa Goli na Lionel Messi.
Wenger amejiliwaza kwa kusema: “Natumai Cech atatupa moyo mkubwa na atamtuliza Messi. Natumai Messi ataweweseka na historia kuwa upande wetu!”
Hata hivyo Barca ya sasa si Messi peke yake kwani Mashambulizi yao ni ya Mtu 3 wakiwepo pia Luis Suarez na Neymar.
-Barcelona na Real Madrid ndio pekee hazijafungwa kwenye UCL Msimu huu.
Hii ni mara ya 3 kwa Arsenal kukutana na Barca kwenye hatua hii ya Mashindano haya na mara zote mbili za, Mwaka 2010 na 2011, walibwagwa nje ingawa 2011 walishinda Mechi ya Kwanza Bao 2-1 kwa Bao za Robin van Persie na Andrei Arshavin.
Arsenal, ambao Miaka 10 iliyopita walibwagwa 2-1 na Barca kwenye Fainali ya UCL ambayo Kipa wao Jens Lehmann alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu mapema kwenye Fainali hiyo, wanajipa sana moyo pale Meneja wao Wenger alipoeleza: “Barca ndio ‘Washindi Watarajiwa’ hivyo inabidi sisi tucheze Gemu ya juu kabisa. Lazima tuwe na mkazo. Tujiamini na tujitume!”
MTANANGE HUU WA LEO USIKU
Arsenal, ambao walimaliza Nafasi ya Pili kwenye Kundi F nyuma ya Bayern Munich, ndio Timu pekee pamoja na Real Madrid kuingia Hatua za Mtoano za UCL kila Msimu tangu Mashindano haya yatumie Mfumo mpya kuanzia Msimu wa 2003/04.
Lakini katika Misimu Mitano iliyopita, Arsenal wamekuwa wakitupwa nje kwenye hatua hii.
Barcelona, waliomaliza Washindi wa Kundi E mbele ya AS Roma, wamekuwa wakitinga Hatua za Mtoano za UCL kwa Misimu 12 hadi sasa na wamefika Nusu Fainali mara 7 kati ya 8 zilizopita.

RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
JUMANNE 23 FEB 2016
Mechi kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
Arsenal vs Barcelona
Juventus vs Bayern Munich
No comments:
Post a Comment