Iturbe, mwenye Miaka 24 na ni Mchezaji kutoka Argentina, ilikuwa nusura aende Watford lakini Bournemouth wakatia mkono haraka na kumchota.
Kutoka Stamford Bridge, zipo ripoti kuwa Chelsea inataka kumnunua Straika wa FC Basel Breel Embolo mwenye Miaka 18 ili kuziba pengo la Loic Remy na Radamel Falcao ambao wanatarajiwa kuondoka Mwezi huu Januari.
Inasemekana FC Basel wako tayari kumuuza Embolo ikiwa Chelsea watatoa Pauni Milioni 20.
Embolo huichezea Timu ya Taifa ya Switzerland na ameifungia FC Basel Bao 16 katika Mechi 47 za Ligi.
![](https://metrouk2.files.wordpress.com/2015/11/ad_187157547-e1446974490149.jpg?w=748&h=468&crop=1)
Nao Arsenal wanadaiwa kuwa na nia ya kumsaini Straika wa Napoli Lorenzo Insigne mwenye Miaka 24.
Wakala wa Insigne, Antonio Ottaiano, ameiambia Radio Kiss Kiss Napoli kuwa Paris Saint-Germain na Arsenal zimeonyesha nia ya kumsaini Straika huyo.
Huku wakitoka kwenye Mwezi mbovu kabisa katika Historia yao ya Miaka 138, Meneja wa Manchester United Louis van Gaal sasa anataka kununua Straika katika Dirisha la Uhamisho la Mwezi huu Januari.
Wakiwa wamefunga Bao 25 tu katika Mechi zao 25 zilizopita na pia kuambua Sare 7 za bila Magoli Msimu huu, 6 zikiwa Uwanjani Old Trafford, na pia kufungwa katika Mechi zao 4 zilizopita, 3 zikiwa za Ligi, Van Gaal ameona Straika mpya ndio Mwarobaini wa tatizo lao.
Hivi sasa tegemezi kubwa kwa ufungaji kwa Man United ni Kepteni wao Wayne Rooney na Anthony Martial ambao Msimu huu kila mmoja amefunga Bao 7.
Ijumaa, Van Gaal alifupisha Mkopo wa Chipukizi Will Keane, mwenye Miaka 22, kwa Preston na kumrudisha Old Trafford ili kuimarisha mashambulizi.
Van Gaal ametamka: “Kufunga Mabao ni kipaji. Tunacho hicho kipaji lakini Wachezaji hawajiamini hivi sasa na pengine itabidi tununue Straika mwingine!”
Akielezea matatizo yao, Van Gaal alisema: “Tatizo letu ni ufungaji. Ukitathmini Mechi zetu zote utaona tumeweza kucheza Staili yetu. Ukiondoa Mechi na Arsenal, na Kipindi cha Kwanza dhidi ya Stoke na Palace, hizo hatukucheza Mpira wetu.”
Man United walifungwa na Arsenal na Stoke na kutoka Sare na Palace.
Aliongeza: “Mechi zote zilizobaki tulicheza Mpira wetu na kutengeneza nafasi, kutawala lakini hatukufunga. Tunahitaji pia Straika awe na bahati. Wachezaji wengi hucheza nafasi hiyo na wanapata nafasi ya kufunga na hawafungi, huweza kueleza hilo.”
Van Gaal amesema: “Tungeweza kuwabakisha Mastraika wote lakini tungekuwa na Mastraika wengi kwenye Benchi. Watakosa furaha na kutaka kuondoka. Hiyo ndio hadithi ya Chicharito. Anataka kucheza”
No comments:
Post a Comment