![www.bukobasports.com](https://metrouk2.files.wordpress.com/2015/04/football-leicester-citys-jamie-vardy-celebrates-after-scoring-their-first-goal.jpg)
Vardy, mwenye Miaka 28 na ni Straika hatari wa Leicester City, ndie anaefungana na Romelu Lukaku kwa Ufungaji Mabao katika Ligi Kuu England wote wakiwa na Magoli 15 kila mmoja.
Vardy ndie ameibeba Leicester City kuwa juu kwenye Ligi Kuu England wakiwa Nafasi ya Pili Pointi 2 nyuma ya Vinara Arsenal na Msimu huu ameweka Rekodi kwenye Ligi hiyo kwa kufunga Mabao katika Mechi 11 mfululizo za Ligi.
Lakini tangu aweke Rekodi hiyo, Vardy amefunga Bao 1 tu katika Mechi 6 zilizopita.
Ukame huo umeifanya Leicester ipokonywe uongozi wa Ligi baada ya kushindwa kufunga katika Mechi 3 na kuambua Pointi 2 tu katika hizo.
No comments:
Post a Comment