SIR ALEX FERGUSON AMMIMINIA SIFA MCHEZAJI WAKE WA ZAMANI GARY NEVILLE, ASEMA ATALETA MAENDELEO VALENCIA
Sir
Alex Ferguson amemuunga mkono Mchezaji wa zamani wa Manchester United
Gary Neville kufanikiwa kama Meneja mara baada ya kuteuliwa kuiongoza
Valencia ya Spain hadi mwishoni mwa Msimu huu.
Neville,
mwenye Miaka 40, alitumia maisha yake yote ya uchezaji Soka akiwa chini
ya Sir Alex Ferguson huko Manchester United ambako alicheza Mechi 602
na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Englamnd mara 8, FA CUP mara 3, Kombe la
Ligi mara 2 na UEFA CHAMPIONS LIGI wakati akiwa Mchezaji kati ya 1993 na
2011.
Sir Alex anaamini kipaji cha Gary Neville kilichompa mafanikio kama
Mchezaji na pia Mchambuzi wa Soka kitamsaidia kupata mafanikio kama
Meneja.
Ferguson
ameeleza: “Gary ana sifa nyingi zinazoonyesha atafanikiwa kama Meneja.
Umahiri kama Kiongozi, uaminifu na uchapa kazi wake. Ni Mtu ambae
haogopi kufanya maamuzi makubwa na hiyo ni sifa kubwa kwa Mtu
anaeongoza. Nadhani atafanya vizuri na namtakia yeye na Ndugu yake Phil,
kila la heri.”
Neville, ambae pia aliichezea England mara 85,
aliteuliwa kuwa Meneja mpya wa Valencia hapo Jana na Mmiliki wa Klabu
hiyo ya La Liga Peter Lim ambae ni Tajiri kutoka Singapore ambae pia ni
Rafiki wa Neville.
Uteuzi huo ulimfanya Neville ajiuzulu kama
Mchambuzi wa Sky Sports lakini atabaki kama Kocha Msaidizi wa Timu ya
Taifa ya England chini ya Roy Hodgson.
Baada ya kujiuzulu kwa Kocha
Nuno Wikiendi iliyopita baada ya kufungwa 1-0 kwenye La Liga na Sevilla
na kutupwa Nafasi ya 9, Valencia iliwekwa chini ya uongozi wa muda wa
Phil Neville, mdogo wa Gary Neville ambae aliteuliwa kama Meneja
Msaidizi tangu Julai, pamoja na Voro, ambae ndie kaimu Meneja.
Jana
Voro na Phil Nevill waliiongoza Valencia kuifunga Barakaldo 3-1 kwenye
Copa del Rey na pia wataendelea kuiongoza Jumamosi itakapopambana na
Barcelona kwenye La Liga.
Mechi ya kwanza ya Valencia chini ya Gary
Neville itakuwa Desemba 9 dhidi ya Lyon ikiwa ni Mechi ya Kundi H la
UEFA CHAMPIONS LIGI.
No comments:
Post a Comment