Neville, ambae pia aliichezea England mara 85, aliteuliwa kuwa Meneja mpya wa Valencia hapo Jana na Mmiliki wa Klabu hiyo ya La Liga Peter Lim ambae ni Tajiri kutoka Singapore ambae pia ni Rafiki wa Neville.
Uteuzi huo ulimfanya Neville ajiuzulu kama Mchambuzi wa Sky Sports lakini atabaki kama Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya England chini ya Roy Hodgson.
Baada ya kujiuzulu kwa Kocha Nuno Wikiendi iliyopita baada ya kufungwa 1-0 kwenye La Liga na Sevilla na kutupwa Nafasi ya 9, Valencia iliwekwa chini ya uongozi wa muda wa Phil Neville, mdogo wa Gary Neville ambae aliteuliwa kama Meneja Msaidizi tangu Julai, pamoja na Voro, ambae ndie kaimu Meneja.
Jana Voro na Phil Nevill waliiongoza Valencia kuifunga Barakaldo 3-1 kwenye Copa del Rey na pia wataendelea kuiongoza Jumamosi itakapopambana na Barcelona kwenye La Liga.
Mechi ya kwanza ya Valencia chini ya Gary Neville itakuwa Desemba 9 dhidi ya Lyon ikiwa ni Mechi ya Kundi H la UEFA CHAMPIONS LIGI.
No comments:
Post a Comment