Rais wa klabu ya Sunderland ya nchini England Shot Elis amewaalika viongozi wa klabu bingwa nchini Simba kwenda jijini
London kwa ajili kukamilisha mambo mbalimbali ya kiushirikiano baina ya klabu
zao chini ya mradi wa klabu hiyo wa Invest in Afrika.
Viongozi
hao wa Simba wakiwa jijini London nchini England, pia watapata fursa ya
kuangalia mchezo wa ligi ya soka nchini humo 'Primier League' baina ya
Sunderland na Fulham mchezo utakao fanyika tarehe 02/march/2013.
Hato
yameelezwa na mwenyekiti wa Simba Alhaji Ismail Aden Rage katika
mkutano wake na waandhishi wa habari hii leo katika makao makuu ya klabu
hiyo Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Rage
amesema hatua hiyo imefuatia jitihada zilizofanywa na Rais Jakaya
Kiwete ambaye alimtambulisha Rais huyo wa Sunderland kwa viongozi wa
Simba kabla ya kukutana na mwenyekiti Aden Rage na mfadhili wa Simba
mama Rahma Alharous jumatatu iliyopita na kufanya mazungumzo.
Rage
amesema Rais wa Sunderland awewaahidi kuanzia msimu ujao wa ligi kuu ya
England Simba itakuwa ikipata vifaa mbalimbali vya klabu hiyo kupitia
mradi wa klabu hiyo wa uwekezaji barani Afrika, ambapo vilabu ambavyo
vimekuwa vikipata vifaa hivyo chini ya mradi wa Invest in Afrika
vimekuwa vikipata paund milioni tatu na kwamba hiyo itakuwa ni faida kwa
klabu yake ambapo pia wamekubaliana kuwa Sunderland itakuwa ikitoa
msaada wa kiufundi kiufundi kwa Simba.
Rage
ambaye pia alitumia fursa hiyo kumtambulisha mfadhili wao mpya ambaye
aliifandhili safari ya Simba katika ziara yao ya mazoezi nchini Oman
kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara Bi
Rahma Al Harouz, amesema anaamini kwa ushirikiano ulipo sasa baina yao
na Bi Rahma ambaye anatambulika kama Malkia wa nyuki, na yeye Rage
akimwita mpiganaji basi watafanikisha mambo mengi yenye lengo la kuleta
mabadiliko ndani ya klabu hiyo.
Sambamba
na hilo Rage amesema ndani ya mazungumzo yao yaliyokuwa chanya,
wamekubalina kuwa wachezaji wawili wa Simba, Shomari Kapombe na
Ramadhani Singano 'Messi' waende jijini London, mara baada ya ligi kuu
kumalizika kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka katika klabu hiyo ya
Sunderland.
Simba
tayari imeanza kupokea vifaa kutoka klabu hiyo kongwe nchini England
ambavyo vina maandishi ya utambulisho wa mradi wa uwekezaji wao barani
Afrika wa 'Invest in Afrika'(Tazama picha juu).
No comments:
Post a Comment