Pages

Saturday, November 7, 2015

RATIBA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI HII, MAN UNITED v WEST BROM, STOKE CITY v CHELSEA...JUMAPILI ARSENAL v SPURS, ASTON VILLA v MAN CITY

BAADA ya kuamua kutokata Rufaa kupinga Adhabu yake ya Kufungiwa Mechi 1, Meneja wa Chelsea Jose Mourinho sasa hatakanyaga Britannia Stadium hapo Jumamosi wakati Timu yake ikicheza na Stoke City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Mourinho alipewa Adhabu hiyo ya Kufungiwa Mechi 1 na pia kutokanyaga Uwanjani kwenye Mechi hiyo pamoja na Faini ya Pauni 40,000 juu baada ya tukio lake Chelsea ilipofungwa 2-1 na West Ham hapo Oktoba 24 huko Upton Park.
Licha ya kukatazwa kukanyaga Britannia Stadium, Mourinho atasafiri na Kikosi chake kwenda huko Mjini Stoke-on-Trent na pia kuwajibika na uamuzi wa kubadilisha Wachezaji wakati wa Mechi hiyo.

Akielezea uamuzi wake wa kutokata Rufaa, Mourinho amesema: “Nimeamua kusalimu amri. Ni upuuzi kuamua kupigana wakati unajua utashindwa.”
Alipoulizwa je ataisimamiaje Mechi hiyo wakati hayupo Uwanjani, Mourinho alijibu: “Sina mipango ya kuangalia Gemu hiyo. Labda nitakaa kwenye Kona ya Mtaa na iPad nikifuatilia Mechi.”
Katika Mechi yao ya mwisho ya Ligi, Chelsea walibondwa Nyumbani kwao Stamford Bridge 3-1 na Liverpool, hicho kikiwa kipigo chao cha 6 kwenye Ligi katika Mechi zao 11 na kutupwa Nafasi ya 15.
Lakini Juzi, Chelsea ilishinda ikiwa kwao Stamford Bridge kwa kuichapa Dynamo Kiev 2-1 kwenye Mechi ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Novemba 7

15:45 Bournemouth v Newcastle
18:00 Leicester v Watford
18:00 Man United v West Brom
18:00 Norwich v Swansea
18:00 Sunderland v Southampton
18:00 West Ham v Everton
20:30 Stoke v Chelsea

Jumapili Novemba 8
16:30 Aston Villa v Man City
19:00 Arsenal v Tottenham
19:00 Liverpool v Crystal Palace

No comments:

Post a Comment