Pages

Saturday, November 7, 2015

DIEGO COSTA NDANI YA KIKOSI CHA SPAIN KITAKACHOUMANA NA ENGLAND NA BELGIUM.

FOWADI wa Chelsea Diego Costa amerudishwa kwenye Kikosi cha Spain chini ya Kocha Vicente del Bosque kwa ajili ya Mechi za Kirafiki dhidi ya England na Belgium zitakazochezwa baadae Wiki ijayo. Kocha Vicente del Bosque ametangaza Majina ya Wachezaji 24 kwa ajili ya Mechi hizo na yumo Diego Costa ambae Mwezi uliopita hakuitwa Kikosini wakati Spain inamaliza Mechi za Kundi lao la EURO 2016 hasa kwa sababu alikuwa Kifungoni.
Uteuzi wa Costa kuichezea tena Spain uliingia hatihati baada ya Del Bosque kumponda Fowadi huyo Mzaliwa wa Brazil kwa kushitakiwa na FA, Chama cha Soka cha England, kwa Utovu wa Nidhamu kufuatia vurugu zake kwenye Mechi ya Ligi na Arsenal Mwezi Septemba na kisha kufungiwa.
Costa, mwenye Miaka 27, ameichezea Spain mara 11 na kufunga Bao 1 tu lakini pia Msimu huu akiwa na Klabu yake Chelsea amefunga Bao 3 katika Mechi 14.
Spain watacheza na England huko Alicante, Spain hapo Novemba 13 na kisha kusafiri kwenda Brussels Siku 4 baadae kuwavaa Wenyeji Belgium.

KIKOSI KAMILI:
KIPA: Iker Casillas (Porto/POR), David de Gea (Manchester United/ENG), Sergio Rico (Sevilla/ESP)

MABEKI: Juanfran (Atletico Madrid/ESP), Mario Gaspar (Villarreal/ESP), Sergio Ramos (Real Madrid/ESP), Gerard Pique, Marc Bartra, Jordi Alba (Barcelona/ESP), Cesar Azpilicueta (Chelsea/ENG), Mikel San Jose (Athletic Bilbao/ESP)

VIUNGO: Sergio Busquets, Andres Iniesta (Barcelona/ESP), Santi Cazorla (Arsenal/ENG), Cesc Fabregas (Chelsea/ENG), Isco (Real Madrid/ESP), Thiago Alcantara (Bayern Munich/GER), Juan Mata (Manchester United/ENG), Koke (Atletico Madrid/ESP)

MAFOWADI: Pedro Rodriguez, Diego Costa (Chelsea/ENG), Paco Alcacer (Valencia/ESP), Nolito (Celta Vigo/ESP), Alvaro Morata (Juventus/ITA)

No comments:

Post a Comment