Msanii nyota wa Afrika Kusini, Bo Denim "Bo" akitumbuiza jukwaani wakati wa tamasha la msimu wa pili la Karibu Music Festival..!
Na Andrew Chale, Modewjiblog
Mwanamuziki
nyota kutoka Afrika Kusini Bo Denim maarufu ‘Bo’ amewashukuru waandaji
wa tamasha la Music Festival linalofanyika kila mwaka mjini hapa huku
likihusisha vikundi na wanamuziki mbalimbali kutoka mataifaa tofauti ya
Afrika nan je ya Afrikaa.
Bo ambaye usiku wa jana Novemba 7,
aliweza kupiga shoo hiyo kwa kiwango cha Kimataifa, alipata shangwe
kwa mashabiki waliofurika kushuhudia tamasha hilo mjini hapa.
Baada ya shoo hiyo Modewji ilipata
kufanya naye mahojiano ambapo amepongeza muziki wa Tanzania wakiwemo
wasanii wanaovuma nje ya mipaka ya Tanzania. “Wasanii wa Tanzania
wanauwezo mkubwa. Nimeshuhudia kundi la Weusi wamefanya vizuri sana”
ameeleza Bo.
Tamasha hilo ambalo leo Novemba
8.2015, linatarajiwa kufikia tamati, linaratibiwa na Karibu Cultural
Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and
Promotions Co. Ltd, T kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel
Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precision Air,
Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor,
Jovago, Kaymu na Time tickets.
No comments:
Post a Comment