Pages

Tuesday, November 3, 2015

JOSE MOURINHO AFUNGIWA MECHI 1 NA FAINI

MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amefungiwa Mechi 1 kutokanyaga kabisa Uwanjani na pia kulipa Faini ya Pauni 40,000 Adhabu ambazo zimetolewa na FA, Chama cha Soka England.
Adhabu hizi, ambazo zinaanza mara moja, zinahusiana na Shitaka la Utovu wa Nidhamu wakati wa Mechi waliyofungwa na West Ham hapo Oktoba 24.
Kwenye Mechi hiyo, Refa Jon Moss alimpa Kadi Nyekundu Mourinho baada ya Meneja huyo kutaka kuingia Chumba cha Marefa wakati wa Haftaimu.
Kipindi cha Pili chote cha Mechi hiyo, Mourinho alikaa Jukwaa la Watazamaji.
Kifungo cha Mourinho kinamaanisha Jumamosi Novemba 7 haruhisiwi kutia mguu Britannia Stadium wakati Stoke City inacheza Mechi ya Ligi Kuu England na Chelsea.

No comments:

Post a Comment