Pages

Wednesday, November 11, 2015

CRISTIANO RONALDO NA BENITEZ WASIWASI MTUPU

Cristiano Ronaldo sasa ‘hajisikii’ Klabuni Real Madrid kwa mujibu wa Wanahabari wa Spain huku hatima yake ikiwa haijulikani.
Jana Ronaldo alikuwa Jijini London katika uzinduzi wa Filamu ya Maisha yake iitwayo ‘Ronaldo’ na Magazeti ya huko Spain, likiwemo lile la kuaminika Marca likitoa ripoti kutokuwa na maelewano kati ya Mchezaji huyo na Kocha wa Real Rafa Benitez.
Pia ripoti hizo zimedai Ronaldo anajihisi kutopewa heshima anayostahili kwenye Timu ya kuwa yeye ni Mchezaji mkubwa.
Hayo yote yamefanya, kwa mujibu wa ripoti hizo, Ronaldo kupooza kwenye Mechi za Real hivi karibuni.
Gazeti la Marca, ambalo lina mwegemeo wa Real huko Jijini Madrid, limeandika kuwa Ronaldo ‘hajisikii’ hapo Real Madrid na sababu kubwa ni Rafa Benitez hasa kutokana na staili ya uchezaji ya Kocha huyo.
Alipohojiwa Jumatatu kuhusu nini kitajiri baadae kwake yeye huko Real, Ronaldo alisema: “Bado nina Miaka Miwili kwenye Mkataba wangu na Real lakini huwezi kujua nini kitatokea baadae.”

Mbali ya Gazeti la Marca, pia stori hizi hizi za Ronaldo ziliwekwa kwenye Magazeti makubwa ya huko Spain likiwemo AS huku Mundo Deportivo likimkandya na kutoa takwimu kuwa Neymar wa Barcelona sasa ana Bao 11 kwenye La Liga wakati Ronaldo ana Bao 8 wakidokeza pia kuwa Mbrazil huyo atampiku Ronaldo kwenye kinyang’anyiro cha Ballon d'Or Mwezi Januari.

No comments:

Post a Comment