Pages

Wednesday, November 11, 2015

CHELSEA NA WEST HAM UNITED ZALIMWA FAINI NA FA'

Klabu za West Ham na Chelsea zimetozwa faini ya £40,000 na £50,000 mtawalia na Shirikisho la Soka la Uingereza baada ya kukiri mashtaka ya utovu wa nidhamu.
Adhabu hiyo imetokea kufuatia yaliyojiri wakati wa ushindi wa West Ham wa 2-1 dhidi ya Chelsea uwanjani Upton Park Oktoba 24.
Wachezaji watano wa Chelsea walilishwa kadi za manjano na na kiungo wa kati Nemanja Matic na meneja Jose Mourinho walifukuzwa uwanjani.
Wachezaji wa West Ham walimzingira refa Jonathan Moss baada ya Matic kumkaba Diafra Sakho dakika ya 44.
“Shtaka lilihusu kukosa kuhakikisha wachezaji wanadumisha nidhamu uwanjani,” FA imesema kupitia taarifa.

“Klabu zote mbili pia zimeonywa vikali dhidi ya kurudia hayo siku za usoni.”
Wachezaji wa Chelsea pia walimzingira refa baada ya Matic, aliyeonyeshwa kadi ya njano awali, kupewa kadi nyingine ya njano na Moss na kufukuzwa uwanjani.

Mourinho alifukuzwa eneo wanamokaa marefa kipindi cha pili baada yake kwenda kumzungumzia Moss chumbani mwake wakati wa mapumziko.
Alipigwa marufuku uwanjani mechi moja na kupigwa faini ya £40,000.

No comments:

Post a Comment