Pages

Thursday, September 3, 2015

KUZIONA STARS NA SUPER EAGLE 7000



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema kiwango cha chini cha kuziona Taifa Stars dhidi ya Nigeria (Super Eagles) ni 7000.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Afisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto alisema maandalizi ya mchezo huo utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam yamekamilika.
“Viingilio vya mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON Qaulifier 2017) kundi G itakua ni VIP A 40,000, VIP B 30,000, VIP C 15,000, Rangi ya Machungwa (Orange) 10,000, na viti vya rangi ya Bluu na Kijani 7,000”, alisema Kizuguto.
Pia Kizuguto alisema tiketi za mchezo huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo saa 4 kamili asubuhi katika vituo kumi ambavyo ni
Ofisi za TFF – Karume, Buguruni – Oilcom, Mbagala – Dar live, Ubungo – Oilcom, Makumbusho – Stendi, Uwanja wa Taifa, Mwenge – Stendi, Kivukoni-  Feri, Posta – Luther House na Big Bon – Msimbazi Kariakooo
Kizuguto alisema TFF inawaomba watanzania, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu kununua tiketi za mchezo huo katika magari yaliyopo kwenye vituo vilivyotajwa ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.
Pia alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na idara nyingine za kiusalama wameandaa usalama wa kutosha kuelekea kwenye mchezo huo na kuhakikisha kila mpenzi wa mpira wa miguu anaingia kushuhudia mchezo na kuondoka salama.
Mchezo huo utaanza saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika na kocha Mkwasa ameendelea na mazoezi jana asubuhi na jioni katika Uwanja wa Taifa kabla ya kufanya mazoezi mepesi ya mwisho leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment