Pages

Thursday, September 3, 2015

DE GEA KUTOKWENDA REAL, MAN UNITED YATOA TAMKO KALI

Manchester United wametoa Taarifa kuhusu Uhamisho ulioshindikana Dakika za mwisho kwa Kipa wao David De Gea kuhamia Real Madrid baada ya kulaumiwa na kukana kabisa kuwa si kosa lao. Mapema Leo Real Madrid walitoa Taarifa yenye Vipengele 10 wakiwashutumu Man United kwa kuchelewesha Uhamisho hadi Dirisha la Uhamisho kufungwa huko Spain.
Kutokana na hilo, De Gea anabaki Mchezaji wa Man United hadi mwishoni mwa Msimu huu Mkataba wake utakapomalizika.
IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI YA MAN UNITED:
Manchester United inafahamu kuhusu Taarifa ya Real Madrid kuhusu jaribio lao kumsaini David De Gea na kumuuza Navas kwa Manchester United. Klabu imepata msukumo kutoa ufafanuzi kwa ukweli ufuatao:
-Manchester United haikuwatafuta Real Madrid kuhusu kumuuza David. David ni Mchezaji muhimu kwa Klabu na matakwa ya Klabu ni kutomuuza.
-Hakuna Ofa yeyote iliyopokelewa kwa ajili ya David hadi Jana.
-Jana Mchana, Real Madrid walitoa Ofa ya kwanza kumnunua David. Dili ikakubaliwa kati ya Klabu mbili ambayo pia ilihusu Navas kuhamia Old Trafford. Dili hii ilitegemea vitu hivyo viwili.
-Katika Masaa ya mwisho, Navas akiwa kambi ya mazoezi ya Real Madrid, wao ndio walikuwa wakihodhi Makabrasha yote ya David, Navas na Real Madrid. Manchester United wao walikuwa tu na Makabrasha ya Manchester United.
-Manchester United walituma Makabrasha ya Uhamisho kwa Wachezaji wote Wawili kwa Real Madrid Saa 20:42, Saa za Uingereza. Mikataba ya David ikarudishwa na Real Madrid bila ya kuwa na Ukurasa wa Saini Saa 2232, Saa za Uingereza.

-Saa 2240, Saa za Uingereza, zikibaki Dakika chache kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa huko Spain, yakaja mabadiliko makubwa kwenye Mikataba na kuhatarisha kukamilika kwake.

-Ilipofika Saa 2255, Saa za Uingereza, ndipo Mikataba yote iliyokamilika kuhusu David ikatumwa kwetu na Real Madrid.

-Wakati huo, Mikataba ya Navas ilikuwa haijarudishwa na Real Madrid.


-Saa 22:58, Saa za Uingereza, Makubaliano ya Uhamisho yakatumwa na Manchester United na kuingizwa kwenye Mtandao wa FIFA wa Uhamisho wa Kimataifa, TMS [Transfer Matching System] na kukubalika, ikiwa ni kabla ya Dirisha la Uhamisho kufungwa.

-Tunachoelewa Dili hii haikukamilika kwa sababu ya:

-Real Madrid walichelewa kuingiza Mikataba ya David kwenye Mtandao wa TMS kwa wakati.

-Real Madrid walichelewa kuingiza Mikataba ya David kwenye Mtandao wa Wasimamizi wa Ligi ya Spain, LFP, na kufuatana na ripoti, walifanya hivyo Dakika 28 baada ya muda kupita.

-Ukweli kwamba Manchester United waliingiza Mikataba yote kwenye Mitandao ndani ya wakati umekubaliwa na FA, Chama cha Soka England ambao wako tayari kusapoti hata kwa FIFA.

-Manchester United ilitaka kuwapa ufafanuzi Real Madrid kuhusu utumwaji wote wa Makabrasha kwa wakati lakini wao wamekataa kusikiliza hili.

-Manchester United hushughulikia Uhamisho wakati wote kwa weledi mkubwa.

-Klabu inafurahia Mchezaji anaependwa na Mashabiki na kuteuliwa Mchezaji Bora wa Mwaka anabakia Mchezaji wa Manchester United.

No comments:

Post a Comment