Pages

Tuesday, September 1, 2015

MARTIAL ATUA OLD TRAFFORD

Straika wa AS Monaco Anthony Martial akaribishwa Manchester United kwenye Dili ya Pauni Milioni 36 ambayo itamfanya awe Tineja wa Bei ghali mno.
Hivi sasa Kijana huyo wa Miaka 19 ambae ameitwa Kikosi cha Timu ya Taifa ya France anafanyiwa upimwaji afya yake huko Man United.
Wadau wengi wa Man United wamekuwa wakijiuliza Anthony Martial ni nani lakini ni Kijana Fowadi hatari ambae anafananishwa na Thierry Henry kiasi cha Kocha wa France Didier Deschamps kuamua kumwita Timu ya Taifa.Martial alianza Soka lake kwenye Chuo cha Soka cha Lyon na kuichezea Timu ya Kwanza Mechi 3 kisha kuhamia AS Monaco Mwaka 2013 kwa Pauni Milioni 3.6.

Msimu uliopita, Martial ndio aling’ara sana na kuipigia AS Monaco Bao 11.

Moja ya Mechi zake alizowika ni ile ya waliyoibwaga Arsenal nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwa kuichapa 3-1 huku Martial akimgeuza atakavyo Hector Bellerin.

Hata UEFA, kwenye Ripoti yao ya Ufundi ya Mwaka 2013, kufuatia Fainali za EURO 2013 kwa U-21, ilimtambua na kumtaja kuwemo katika Kikosi Bora cha Mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment