Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, September 30, 2015

MANCHESTER UNITED KIBARUANI LEO NA WOLFSBURG KWENYE UEFA CHAMPIONS



Memphis Depay akiteta jambo kwa furaha na Rooney leo wakati wa Mazoezi kwenye uwanja wao wa Aon Training Complex huko Carrington. Man United wanajiandaa na kukwaana na Timu ya Wolfsburg kwenye UEFA Champions League ;leo jumatano. Mchezo utakaopigwa Old Trafford usiku.
Jumatano Usiku Uwanjani Old Trafford, Manchester United watacheza na Klabu ya Germany VfL Wolfsburg katika Mechi ya Pili ya Kundi B la UEFA CHAMPIONS, Kwenye Mechi za kwanza za Kundi B, Man United ilifungwa 2-1 na PSV Eindhoven huko Holland na Wolfsburg kuitungua CSKA Moscow 1-0 huko Germany.

Kipa wa Manchester United David de Gea na Juan Mata wakiwa pamoja kumbuka wanakuwa pamoja muda mwingi kwa kuwa Lugha ya Mata na De Gea inaendana na kesho wanawakaribisha Wolfsburg. Mchezo wa Mwisho wa Man United walifungwa 2-1 na Timu ya PSV Eindhoven mapema mwezi huu kwenye mechi ya Ufunguzi. Mchezo ambao pia uliwaachia pengo kubwa la Luke Shaw kwa kuumizwa vibaya Mguu wake.
Wakati Man United wanatinga kwenye Mechi hii wakitoka kuitwanga Sunderland 3-0 na kutwaa uongozi wa Ligi Kuu England, Wolfsburg wao wamekosa ushindi katika Mechi zao mbili zilizopita kwa kwenda Sare 1-1 na Hannover 96 na kutandikwa 5-1 na Bayern Munich kwenye Mechi ambayo Robert Lewandowski aliweka Rekodi kwa kupiga Bao zote hizo 9 ndani ya Dakika 9 tu za Kipindi cha Pili.Rooney na Schweinsteiger wakiteta jambo huku furaha ikiwa imewafungukia kwa asilimia kubwa na Kesho wanatarajia kuonesha uzoefu wao katika harakati za kutaka kuibuka na ushindi.

Schweinsteiger tena na Ashley Young.
Depay, Morgan Schneiderlin, Schweinsteiger na Rooney leo wakati wa mazoezi yao.

Rooney akiwaongoza wenzake leo wakati wa mazoezi akiwa sambamba na Schweinsteiger na Depay. kulia nyuma ni Meneja wao Van Gaal akiwaangalia vyema kuona Vijana wake wataweza kumaliza mazoezi vyema na kujiandaa na kipute hicho cha kesho ambacho ni Muhimu kushinda wakiwa pia nyumbani kwao Old Trafford.

No comments:

Post a Comment