Pages

Friday, September 18, 2015

LUKE SHAW KUFANYIWA OPERESHENI YA PILI LEO EINDHOVEN

BEKI wa Manchester United Luke Shaw anatarajiwa kufanyiwa operesheni ya pili Ijumaa kutibu Mguu wake wa Kulia uliovunjika Mifupa yote miwili kwenye ugoko.
Shaw aliumizwa na Beki wa PSV Eindhoven Hector Moreno katika Dakika ya 15 ya Mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Jumanne Usiku huko Netherlands wakati Man United wanafungwa 2-1 na PSV na kupelekwa Hospitali ya St Anna Ziekenhuis iliyoko nje tu ya Jiji la Eindhoven na Usiku huo huo kufanyiwa operesheni iliyosimamiwa na Madaktari Wawili Mabingwa wa Mifupa na Mtaalum wa Ajali.

Ingawa Klabu ya Man United imekataa kutoa ufafanuzi kuhusu hali ya Mchezaji wao lakini inaaminika Operesheni ya Pili itafanyika Ijumaa Hospitalini hapo hapo St Anna Ziekenhuis na atabaki hapo hadi itakapoamuliwa na Madaktari kuwa ni salama kusafiri kurudi Manchester.
Mkurugenzi Mtendaji wa Man United, Ed Woodward, ameshamtembelea Shaw na Wazazi wake wamesafirishwa kumwona Mtoto wao.
Habari njema ni kuwa Shaw alivunjika Mifupa hiyo ya Mguuni bila kuwa na athari nyingine za kando na hili limeleta matumaini kupona kwake ni kitu cha wakati tu bila matatizo mengine.
Hata mwenyewe Shaw ameleta matumaini kwa kuposti Mitandaoni maendeleo yake ambayo pia hata Meneja wa Man United Louis van Gaal amegusia kuwa huenda Kijana huyo wa Miaka 20 akarejea dimbani mapema zaidi Machi Mwakani.

No comments:

Post a Comment