Pages

Wednesday, September 16, 2015

ARSENAL YAPATA PIGO, WILSHERE ‘KUPASULIWA’, KUKAA NJE HADI DESEMBA


Arsenal imethibitisha kuwa Kiungo wao Jack Wilshere atafanyiwa upasuaji na atakuwa nje kwa Miezi Mitatu Zaidi.
Wilshere, mwenye Miaka 23, amekuwa akizongwa na majeruhi ya mara kwa mara katika maisha yake yote ya Soka na Msimu huu bado hajaanza kuichezea Arsenal baada ya kuumia Siku moja tu kabla Arsenal kucheza Mechi ya Ngao ya Jamii na Chelsea hapo Agosti 2.Awali ilidhaniwa Wilshere atapona hiyo Enka yake iliyopata ufa mdogo kwenye mfupa wake wakati akiwa mazoezini bila kupasuliwa na angerejea kilingeni Septemba 12 na hilo kutangazwa na Meneja wa Arsenal Arsene Wenger.
Lakini hilo likashindikana na sasa Wilshere ameambiwa anahitaji Operesheni kwenye Enka yake.
Hii Leo Arsenal imetoa taarifa rasmi kuthibitisha kuhitajika kwa upasuaji huo ambao utamweka nje takribani Miezi Mitatu.


Hili ni pigo kubwa kwa Mchezaji huyo na Arsenal ambae Msimu uliopita alianza Mechi 14 tu za Ligi Kuu England baada ya kuwa nje kuuguza Enka yake na kurejea Uwanjani Mwezi Mei karibu Msimu kumalizika.
Mchezaji mwingine wa Arsenal ambae ni Majeruhi na ambae awali alitegemewa atapona hivi hivi tu na baada ya kuchelewa ikaamuliwe nae apasuliwe Goti lake ni Straika Danny Welbeck ambae nae yuko nje hadi baada ya Krismasi.

No comments:

Post a Comment