TIMU ya taifa ya Wanawake, ‘Twiga
Stars’ imeondoka leo kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya kambi ya kujiandaa
na fainali za Matifa ya Afrika “All African Games’ zinatarajiwa kufanyika
nchini Congo Brazaville Septemba mwaka huu.
Akiongea kabla ya kuondoka, Kocha
Mkuu, Rogasian Kaijage alisema anashukuru kwani wachezaji wake wanabadilisha
mazingira jambo ambalo linaweza kuleta matokeo mazuri kwake japo mazoezi ni
yale yale.
“Nimefurahi wachezaji kuondoka
kwenye mazingira ya hapa kwani yana mwingiliano wa watu sana kiasi kamba
wachezaji hawapumziki ipasavyo kwani mara kaja huyu kuzungumza nao hivyo kuwa
mbali italeta utulivu kiasi Fulani”, alisema Kaijage.
Twiga
Stars ambayo imefuzu kwa Fainali za Michezo ya Afrika itakayoanza kutimua vumbi
Septemba 04 – 17 imepangwa kundi A na wenyeji Congo Brazaville na Nigeria
pamoja na Ivory Coast.
Wakati
huo huo, katika kujiweka sawa baada ya kukosa michezo ya kimataifa ya kirafiki,
Twiga ilicheza na timu ya Ilala Academy ya U-17 na kufungwa mabao 3-0 kwenye
Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Mchezo
huo ambao ulivuta mashabiki wengi ambao walikuwa wanasubiri kuona mazoezi ya
Yanga, uliwavutia mashabiki na kuwafanya kuwashangilia kwani walikuwa wakicheza
kwa akili sana kuliko kutumia nguvu.
Mabao
ya Ilala Academy yalifungwa na Rajabu Ally ambaye alifunga mabao mawili na
msumari wa mwisho ulipigiliwa na Hamza Rajab.
No comments:
Post a Comment