Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 11, 2015

LULI KAYAGE AMPIGA LIZBETH KWA KO AFRIKA KUSINI



BONDIA Lulu Kayage ameibuka kidedea baada ya kumpiga wa KO bondia  Lizbeth Sivhaga wa Afrika Kusini.
Pambano hilo lilifanyika juzi kwenye mji wa Limpopo ni pambano la kwanza kwa Lulu kucheza nje ya nchi na kufanikiwa kushinda kwa K.O katika raundi ya pili.
 Akizungumza baada ya kuwasili nchini, Rais wa TPBO, Yasin Ustaadhi Abdallah ambaye alambatana na bondia huyo, alisema kuwa mchezo huo ulioanza kwa kasi huku kila mmoja akionesha mashambulizi kutaka kumpiga mwenzie katika raundi za awali.
“Pambano lilikuwa zuri kwani kila mmoja akionesha nia ya kumpiga mwenzake lakini ilivyofika raundi ya pili bondia Lulu alimwelemea sana mpinzani wake kwa makonde mfululizo na wasaidizi wake kumuokoa kwa kumtupia taulo hivyo Lulu alishinda K.O ya raundi ya pili”, alisema Yasin.
Pia Yasin alisema bondia Ramadhani Shauri amepoteza pambano wake kwa kupigwa K.O ya raundi ya nne na bondia Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini, pambano ambao ulikuwa wa raundi nane.
Naye bondia Lulu amewashukuru watanzania kwa dua zao kwani haikuwa kazi rahisi kupambana na kushinda ukiwa ugenini, pia alimshukuru kocha wake Habibu Kinyogoli kwa mbinu ambazo amekuwa akimpa hadi kufikia hapo alipo.

No comments:

Post a Comment