Pages

Saturday, August 29, 2015

LIONEL MESSI ATWAA TUZO YA UEFA MSIMU 2014/2015

Lionel Messi ametwaa Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa Msimu wa 2014/15 baada ya kushinda Kura zilizopigwa na Wanahabari toka Nchi 54 Wanachama wa UEFA.
Messi, mwenye Miaka 28, ametwaa Tuzo hii kwa kuwabwaga mwenzake wa Barcelona Luis Suarez na Mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ambae ndie Mchezaji Bora Duniani.
Hii ni mara ya pili kwa Messi kutwaa Tuzo hii na mara ya kwanza ni Mwaka 2011 na safari hii ameibeba baada ya kuisaidia Klabu yake Barca kutwaa Trebo yaani Ubingwa wa La Liga, Copa del Rey na UEFA CHAMPIONS LIGI. Washindi waliopita wa Tuzo hii ni Lionel Messi (2011), Andrés Iniesta (2012), Franck Ribéry (2013) na Ronaldo (2014).Taswira leo hii huko MonacoSuarezIniesta akiwa amebeba Kombe la UEFA

No comments:

Post a Comment