Kesho jumamosi Chelsea watawakaribisha Swansea Citykwenye mchezo wa kufungua pazia Ligi kuu England na mchezo huo utapigwa Darajani saa moja na nusu usiku kwa saa zetu.
Kibarua kikubwa kwa Chelsea kitatokana na Vigogo Wanne, Manchester City, Arsenal, Manchester United na Liverpool, ambao wamejiimarisha kwa kishindo kwa kununua Wachezaji ngangari wapya.
Hali hiyo imemfanya Jose Mourinho aungame kuwa kutetea Taji lao itakuwa shida kubwa na hilo Wachambuzi wamekubaliana nae hasa baada ya Chelsea kuongeza Wachezaji wawili tu hadi sasa ambao ni Straika wa Mkopo kutoka AS Monaco, Radamel Falcao na Kipa Asmir Begovic huku wakimuuza Kipa wao mahiri Petr Cech kwa Arsenal.
Hata hivyo, Chelsea ikiwa na Mastaa Eden Hazard, Cesc Fabregas na Diego Costa bado ni Timu ngumu.
Hilo limebainishwa pia na Meneja Mpinzani mkubwa wa Mourinho, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ambae amesema: “Mwaka Jana Chelsea walishinda kwa tofauti kubwa hivyo wao wanapewa nafasi kubwa ya Ubingwa. Mwaka Jana, baada ya Gemu 12 tulikuwa Pointi 15 nyuma ya Chelsea lakini katika Gemu zilizobakia tulizoa Pointi 58 na wao 55.”
No comments:
Post a Comment