Pages

Thursday, August 20, 2015

AZAM TV KUONYESHA LIVE MECHI YA YANGA VS AZAM FC


Runinga ya Azam TV itarusha moja kwa moja mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Tanzania Bara dhidi ya Azam FC walioshika nafasi ya pili, msimu uliopita.

Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Azam Media, Mgome Kiwanga amesema mechi hiyo itaonyeshwa moja kwa moja.
“Kweli itaonyesha na hilo ni sehemu ya faida ambazo walio na visimbuzi vya Azam wanaweza kufaidika.
“Pia kutakuwa na uchambuzi wa kina kabla ya mechi hiyo ambao unawapa nafasi wapenda soka kujua mengi zaiid kabla ya mchezo,” alisema Mgope.
Mechi hiyo inayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi, yaani keshokutwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.

No comments:

Post a Comment