Pages

Saturday, July 11, 2015

YOHAN CABAYE AJIUNGA NA KLABU YA CRYSTAL PALACE KWA DAU LA REKODI AKITOKEA PSG!

Crystal Palace imemsaini Mfaransa Yohan Cabaye kutoka kwa Mabingwa wa France Paris St-Germain kwa Dau la Rekodi kwa Klabu hiyo la Pauni Milioni 10.
Cabaye, mwenye Miaka 29, amesaini Mkataba wa Miaka Mitatu na ameshawahi kuchezea Ligi Kuu England akiwa na Newcastle ambayo aliihama Januari 2014 na kwenda PSG.
Lakini huko PSG alianza Mechi 13 tu kwani Meneja Laurent Blanc aliwapa kipau mbele Viungo Thiago Motta, Javier Pastore, Marco Verratti na Blaise Matuidi.
Dau kubwa ambalo Palace waliwahi kulipa kumnunua Mchezaji ni hapo 2014 walipoilipa Wigan Pauni Milioni 7 kumnunua Kiungo wa Scotland James McArthur.

No comments:

Post a Comment