Pages

Sunday, July 5, 2015

TANZANIA YATUPWA NJE CHAN NA UGANDA KWA MABAO 4-1 BAADA YA JANA KUTOKA SARE YA 1-1

Kikosi cha Taifa Stars kilichochuana Vikali na Uganda CranesMashabiki wa Taifa Stars wakitoa sapoti ya nguvu!Bao 1-0 John Bocco na mpira akipeta!
Stars walipata Bao lao kwa Penati ya Dakika ya 58 iliyopigwa kifundi na John Bocco lakini Uganda wakasawazisha dakika ya 82 kupitia Kizito Kezironi alieingizwa punde tu kutoka Benchi na mtanange kumalizika kwa 1-1. Hivyo Taifa Stars wametupwa nje kwa (Agg:4-1). Ushindi huu unawasogeza hatua inayofuata na sasa kukutana na Sudan. Kikosi cha Taifa Stars cha leo kilibadilishwa sana kuliko kile cha awali huko Zanzibar walipachapwa 3-0 huku Uganda kuonekana wako vile vile walivyokuwa.Mapunziko, Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika bado ni 0-0 kwenye Uwanja wa Nakivubo War Memorial Stadium
KIKOSI CHA UGANDA(CRANES)James Alitho -GK [01], Denis Okot Oola [02], Brian Ochwo [03], Hassan Waswa Mawanda-Capt [16], Shafiq Bakaki [14], Derick Tekkwo [08], Muzamil Mutyaba [11], Erisa Sekisambu [17], Farouk Miya [10], John Semazi [07], Robert Sentengo [09].

AKIBA:
Brian Bwete-GK [18], Deus Bukenya [12], Keziron Kizito [06], Yassar Mugerwa [15], Martin Kizza [13], Frank Kalanda [05], Fahad Hassan Muhammad [04]


KIKOSI CHA TAIFA STARS:
Taifa Stars wanaoanza XI: 1. Ally Mustafa ” Barthez”, Shomary Kapombe, Haji Mngwali, Nadir Haroub “Cannavaro”, Kelvin Yondani, Mudathir Yahya , Deus Kaseke, Frank Domayo “Chumvi”, John Bocco, Rashid Mandawa, Saimon Msuva – 12
Akiba: Mudathir Khamis, Juma Abdul, Hassan Isihaka, Salum Telela, Said Ndemla, Ramdhani Singano, Ame Ally.


Tiketi zinauzwa lango kuu na kwenye milango mingine Uwanjani hapo kwa bei hii - 10,000/=(Ordinary), (Covered Stands)20,000/= na VIP 30,000/= kwa bei ya Uganda.Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Uganda

No comments:

Post a Comment