Pages

Tuesday, July 7, 2015

SIMBA YAGARAGAZWA NA MESSI, KUANZI SASA YUPO HURU


Mwenyekili wa kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe na Mjumbe wa kamati ya Utendaji, Collin Frisch wakiondoka kwenye ofisi za TFF baada ya kikao


Mjumbe wa kamati ya Utendaji, Collin Frisch (Kushoto) akiongea na Katibu wa Sputanza
Said George na mchezaji  Ramadhan Singano (kulia) wakiteta baada ya kutoka nje


KLABU ya Simba imeshindwa na mshambuliaji Ramadhan Singano ‘Messi’ kwenye mgogoro wao wa kimkataba ambao umedumu kwa takribani miezi mitatu.

Maamuzi ya mgogoro huo yametolewa mbele ya wandishi wa habari na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Selestine Mwesigwa na kusema Simba imeshindwa kutekeleza masharti ya mkataba ambayo waliagiza wakayafanyie kazi lakini hadi kikao cha jana kinakaa hakuna kilichotekelezwa.

“Awali TFF tulimwita Ramadhan Singano na uongozi wa Simba baada ya kuwasikiliza kila mmoja tukaagiza wakae meza lakini Simba hawakufanya hivyo na shauri hilo likalazimika kupelekwa kwenye kamati ya Maadili, Sheria na Hadhi za wachezaji na maamuzi yametoka kuwa mchezaji Ramadhan Singano yupo huru kuanzia leo”, alisema Mwesigwa.

Mwesigwa alisema Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, iliwakilishwa na mwenyekiti Advocate Richard Sinamtwa na mchezaji Ramadhan Singano alikuwa amefuatana na Mwenyekiti wa Sputanza Mussa Kisoky na katibu Said George wakati Simba iliwakilishwa na Mwenyekili wa kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe na mjumbe wa kamati ya Utendaji, Collin Frisch na Mkurugenzi wa Wanachama wa TFF, Eliud Mvella

Kikao hicho kichukua saa tano kumalizika huku kila upande ukilazimika kutolewa nje wakati upande mwingine ukihojiwa mwishoni upande wa Simba ulitoka ukiwa umenyong’onyea wakati Kisoky na  wenzake walitoka wakicheka huku wakikumbatiana na kuwadokeza waandishi kuwa “Tumeshinda kijana yupo huru ila sisi si wasemaji subirini TFF watatoa taarifa kamili”

Baadae gazeti hili lilimtafuta Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe na kuweka wazi kuwa hawajaridhishwa na maamuzi ya kamati hiyo hivyo watakutana ili kujua hatua zaidi za kuchukua ikiwezekana watakata rufaa kwenye kamati ya Usuluhishi ya mambo ya michezo (CAS) ambayo ipo chini ya Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA).

“Tuliwasilisha ushahidi wote mbele ya Kamati, tumeonyesha mshahara wake ulikuwa kiasi gani na tumeonyesha kwa nini alikuwa anapewa laki moja (100,000) zaidi.
Ili akalipie kodi ya nyumba, lakini bado hatukueleweka. Tunaamini hapa si mwisho, vipo vyombo vingine ambavyo vitatupa haki yetu, tunakwenda kukutana kuangalia uwezekano wa kulipeleka suala hili huko

Kamati ya Sinamtwa imejiridhisha Messi hakuwahi kupewa nyuma ya kuishi na Simba jambo ambalo ni kinyume cha Mkataba baina yake na klabu hiyo hivyo imemevunja rasm,I mkataba wake na kusema yupo huru kusajiliwa na klabu yoyote.

Messi alikuwa analalamikia Simba kupeleka TFF mkataba wa miaka mitatu wakati yeye alikuwa na mkataba wa miaka miwili na Simba jambo lililoleta utata hadi Sputanza kuamua kumsaidia na hatimaye Messi ameshinda.

Messi alisajiliwa Simba miaka minne iliyopita kwenye Simba B na baadae kuingiwa kwenye kikosi A baada ya uwezo wake kuwaridhisha makocha mbalimbali ambao wamekuwa wakiifundisha Simba kwa nyakati tofauti


No comments:

Post a Comment