Pages

Wednesday, July 15, 2015

RATIBA MSIMU MPYA LA LIGA 2015/2016 YATOKA, KUANZA AGOSTI 22, 2015 TIMU ZOTE UWANJANI, REAL NA BARCA KUANZIA UGENINI

LEO Shirikisho la Soka huko Spain, RFEF, wametoa Ratiba ya Msimu mpya wa 2015/26 ambao utaanza Agosti 22.
Ile Mechi, Bigi Mechi huko Spain iliyobatizwa El Clasico, kati ya Mahasimu Barcelona na Real Madrid, itapigwa Novemba na Marudiano ni Aprili.
El Clasico ya kwanza itakuwa Santiago Bernabeu hapo Novemba 8 na Marudiano ni Aprili 3 huko Nou Camp.
Dabi ya Jiji la Madrid, iliyobatizwa El Derbi Madrileno, kati ya Real na Atletico Madrid itachezwa huko Vicente Calderon Nyumbani kwa Atletico hapo Oktoba 4 na Marudiano ni Santiago Bernabeu Februari 28.

Agosti 22, Siku ya Ufunguzi ya Mechi za La Liga, Real, wakiwa chini ya Meneja mpya Rafa Benitez, wataanza Msimu wao Ugenini kwa kucheza na Timu iliyopanda Daraja Sporting Gijon huko El Molinon Stadium huku
Mabingwa Barcelona wakianza Ugenini na Athletic Bilbao lakini hiyo itakuwa mara ya 3 kwa Timu hizo kukutana kwani wao ndi watafungua dimba Msimu huko Spain kwa kugombea Super Cup hapo Agosti 14 na kkurudiana Agosti 17.

MECHI ZA UFUNGUZI:
Athletic Club vs Barcelona 

Sporting Gijon vs Real Madrid
Rayo Vallecano vs Valencia
Espanyol vs Getafe

Malaga vs Sevilla
Levante vs Celta Vigo

Deportivo vs Real Sociedad
Granada vs Eibar
Real Betis vs Villarreal
Atletico Madrid vs Las Palmas

No comments:

Post a Comment