Na Saleh Ally
Rais wa
Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kwa kiasi gani amekuwa akiumizwa na
vipigo mfululizo ambavyo Taifa Stars imekuwa ikivipata.
Kikwete
ameyesema hayo wakati akilihutubia bunge la Tanzania mjini Dodoma, leo.
Kikwete
amekiri kwamba amekuwa akijisikia vibaya kutokana na Stars kupoteza mechi zake
mfululizo hadi yeye kufikia kuamua kutokwenda uwanjani.
“Kila ukienda
wanafungwa, mwisho ikafikia nikaona hawa wanataka kusema mimi ndiye nina nuksi,
nikaacha kwenda. Hata wakiamua Unguja, nako wanapiga tatu,” alisema na
kuwachekesha wabunge.
Lakini baadaye
Kikwete aliwataka wahusika akiwa na maana ya TFF kufanya jambo ili kubadilisha
hali hiyo ya kuwa na timu inayofungwa kila mara.
“Lazima
waliangalie hili na kulifanyia kazi kwa kuwa si sahihi,” alisema Kikwete ambaye
itakuwa ni hotuba yake ya mwisho kulihutubia bunge akiwa rais.
Aidha,
aliendelea kusisitiza uamuzi wake wa kurejesha michezo mashuleni ulivyorejesha
ushindani.
Pia
akazungumzia namna muziki na sanaa ya uigizaji inavyopaswa kupewa nafasi kwa
kuwa wakati mwingine fani hizo zimekuwa zikiwaliwaza Watanzania kimataifa kwa
kuwa soka na michezo mingine imefeli.
No comments:
Post a Comment