Pages

Wednesday, July 1, 2015

NGOMA NA ZUTTA WATAMBULISHWA RASMI LEO





MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga Donald Ngoma, amewataka mashabiki wa timu hiyo kusubiri mambo mazuri kutoka kwake ikiwa ni muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo

Ngoma aliyetambulishwa rasmi leo kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga sambamba na beki Joseph Zuttah, alisema amejipanga kufanya kazi kubwa na kuipa mafanikio timu hiyo ili aweze kudumu kwa muda mrefu kama ilivyokuwa FC Platinum.

“Najisikia furaha kucheza Yanga kwa sababu ni klabu kubwa Tanzania nitahakikisha natumia uwezo wangu naipa naongeza mafanikio yaliyopo kwa kushirikiana na wenzangu nilio wakuta,”alisema Ngoma

Kwaupande wake Zuttah alisema ametua Yanga kwa kazi moja tu ya kuendeleza mazuri yaliyofanywa siku za nyuma na amekuja akiwa kamili na kuwataka washabiki wa timu hiyo kumpa sapoti.

“Nimefurai kuona mashabiki wanaipenda sana timu yao kuanzia Jumamosi wakati Yanga ilipocheza na Sports Villa nimehamasika sana kitu ambacho kimenifanya nisijutie maamuzi yangu ya kucheza Tanzania,”alisema Zuttah.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Habari wa Yanga Jerry Muro alisema wachezaji hao wameshamalizana nao kila kitu na tayari wameshawasilisha usajili wao Shirikisho la soka Tanzania TFF, ili waweze kuombewa kibali cha kufanyia kazi.

Ngoma ametua Yanga akitokea FC Platinum ya nyumbani kwao Zimbabwe wakati Zuttah alikuwa akikipiga klabu ya     Medeama  ambao ni mabingwa wa Kombe la FA nchini kwao Ghana.

Baada ya kuwanasa wachezaji hao wawili tayari Yanga imekamilisha idadi ya nyota saba wakimataifa inayotakiwa na Kanuni za TFF nyota wengine wakimataifa ni Haruna Niyonzima,Amissi Tambwe,Kpah Sherman,Andrey Coutinho na Mbuyu Twite.

No comments:

Post a Comment