Pages

Wednesday, July 15, 2015

CECAFA KUENDESHA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI KESHO

Baraza la Vyama Vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kesho Alhamis tarehe 16 Julai, 2015 litaendesha mtihani wa utimamu wa mwili (Pysical test) kwa waamuzi wa watakochezesha michuano ya kombe la Kagame inayoanza mwishoni mwa wiki huu.

Zoezi hilo la utimamu kwa waamuzi watakochezesha mashindano ya Kagame, litafanyika kuanzia saa 2 asubuhi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam litasimamiwa na kamati ya waamuzi yay a CECAFA.

Waamuzi wanaotarajiwa kuhudhuria zoezi hilo ni Ali Ahmed, Suleiman Bashir (Somalia), Ahmed Djama (Djibout), Yetayew Belachew (Ethiopia), Kakunze Herve (Burundi), Davis Omweno, Peter Sabata (Kenya), Issa Kagabo, Hakizimana Louis (Rwanda), Ahemd El Faith (Sudan), Lee Okelo na Mashood Ssali (Uganda), Israel Mujuni na Ferdinand Chacha (Tanzania).

No comments:

Post a Comment