ARTURO VIDAL ATIMKIA BAYERN MUNICH!
Bayern Munich imekubali kulipa Ada ya Uhamisho ya Pauni Milioni 40 ili kumnunua Vidal ambae alitua Juve Mwaka 2011 akitokea Bayer Leverkusen.
Arturo Vidal alikuwa Mchezaji muhimu kwa Juve kwa kuisaidia kutwaa Ubingwa wa Italy mara 4 mfululizo na pia kuwafikisha Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu uliopita.
Marotta ameeleza: "Vidal ametaka kwenda kwingine kama walivyofanya Angelo Ogbonna, Carlos Tevez na Andrea Pirlo."
Hataa hivyo, Moratta amekataa kuthibitisha uvumi kuwa kwenda kwa Vidal Bayern Munich kutamfanya Mario Gotze aende Juve katika Dili hiyo hiyo.
Post a Comment