Shirikisho
la kandanda duniani,FIFA, limekanusha madai kwamba katibu wao
mkuu,Jerome Valcke,alihusika katika kashfa ya ufisadi ambapo hongo ya
mamilioni ya dola ilitolewa.
Kashfa hiyo inachunguzwa na Marekani .FIFA inasema hamna afisa wake yeyote wa ngazi ya juu aliyehusika kwa njia yoyote katika kashfa hiyo.
Waendesha mashtaka wa Marekani wanasema hongo hiyo ilinuiwa kusaidia kununua kura kuiwezesha Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa kombe la dunia lililofanyika mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment