Kocha wa Taifa stars naye alikuwepo sambamba na nahodha wa Taifa stars na mshambuliaji Mbwana Samatta |
Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa,
zitakazokuwa zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali
itakayokua inazikabili.
Uzinduzi huo
wa jezi mpya uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la Golden
Jubilee uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho, uliongozwa
na mgeni rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.
Katika
uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini,
jezi za nyumbani na jezi zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.
Ifuatayo ni
hotuba ya Rais wa TFF , Jamal Malinzi aliyoisoma wakati wa uzinduzi wa
jezi mpya za timu za Taifa, uzinduzi wa tovuti mpya ya TFF na kutunuku
vyeti kwa viongozi mbalimbali, makocha, wachezaji na wadhamini.
Mh Said Mtanda Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
Mzee Said el Maamry Mwenyekiti Msataafu wa FAT
Ndugu Leodeger Tenga Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF na Rais mstaafu wa TFF
Ndugu wageni waalikwa
Ndugu waandishi wa habari
Mabibi na mabwana
Salam aleikum.
Nianze kwa kumshukuru
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha hapa leo na kwa
mafanikio mbali mbali ambayo tumekuwa tukiyapata.Ninakushukuru sana
ndugu mgeni rasmi kwa kuacha shughuli zako kuja kujiunga nasi asubuhi
hii katika shughuli hii.
Ndugu mgeni rasmi,tarehe
08 oktoba 1964 Tanzania ilipata uanachama rasmi wa shirikisho la mpira
wa miguu duniani FIFA. TFF tuliona jambo zito kama hili hatuwezi
kuliacha lipite hivi hivi.Hivyo mwaka jana tuliamua kuenzi maadhimisho
ya miaka 50 ya kujiunga na FIFA kwa kufanya mambo mambo matatu makubwa.
La kwanza ni kutoa vyeti
maalum kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali kwa kutambua mchango wao
uliotukuka katika kuendeleza mpira wa miguu Tanzania.
Leo hii ndugu mgeni
rasmi tutakuomba ukabidhi vyeti hivi kwa wawakilishi wa makundi kadhaa
kwa niaba ya wenzao.Makundi haya ni pamoja na viongozi wa kitaifa
wastaafu,mawaziri wa michezo wastaafu,viongozi waliopita wa TFF?
FAT,wakurugenzi wa idara
ya michezo,wenyeviti na makatibu wa baraza la michezo la taifa,Timuya
Taifa iliyocheza fainali za Afrika mwaka 1980,waamuzi,makocha,wachezaji
wa timu ya Taifa na watangazaji mahiri wa michezo.Jumla tumetunuku vyeti
194.
Kiuhalisia idadi hii ni
ndogo sana ukilinganisha na wingi na uzito wa michango ya wadau mbali
mbali wa mpira katika miaka 50 iliyopita.
Tunaomba Watanzania
wenzetu watuelewe katika hili kuwa hawa tutakaowatunuku vyeti hivi ni
wawakalilisha wa wadau wote wa mpira Tanzania.
Ninaomba tusimame kwa
muda mfupi tuwaombe ewadau wenzetu na viongozi wa mpira wa miguu ambao
wako katika orodha hii na wametangulia mbele ya haki.
Ndugu mgeni rasmi katika
kuenzi miaka 50 ya Tanzania kujiunga na FIFA leo hii pia tutatoa
mchango wa fedha kwa makundi yenye mahitaji katika jamii.
Pesa hizi zinatokana na
makusanyo mbali mbali ikiwemo makusanyo ya mechi ya ngao ya hisani
ifanyikayo kila mwaka. Makundi haya ni pamoja na walemavu wa
viuongo,walemavu wa ngozi na wasioona.
Kitendo hii ni moja ya
juhudi za TFF kurudisha katika jamii kile tunachokusanya. Kila kundi
litapewa shilingi milioni tano na tunaendelea kupokea maombi toka
makundi mbali ya kijamii na tukiyapitisha tutaendelea kugawa fedha hizi.
Jambo la tatu tutakalolifanya leo litakuwa ni kuzindua rasmi tovuti mpya ya TFF (www.tff.or.tz).
Tumeamua kufanya jamabo hili katika kuenzi miaka hamsini ya kujiunga na
FIFA ili kutoa msisitizo kuwa sasa TFF na sisi tunajiunga Na kuendeleza
mpira kisasa kulingana na teknolojia iliyopo.
Kupitia tovuti hii wadau
wa mpira watapata fursa ya kuhabarishwana kuelimishwa nkuhusu masuala
mbali mbali yahusuyo mpira wa miguu.
Tovuti hii itakuwa pia
na sehemu ya kumbu kumbu (archive) zihusuzo historia ya mpira wa miguu
na matukio mbali mbali katika historia ya mpira wetu.
Tunaomba wadau wenye
kumbu kumbu mbali za mpira kama picha,takwimu,vipande vya magazeti ya
zamani na kadhalika mtuletee ili viingizwe katika tovuti yetu.
Tunaamini tovuti hii itakuwa ndio chanzo kikuu cha taarifa na rekodi mbali mbali za sasa na za zamani zihusuzo mpira wa miguu.
Ndugu mgeni rasmi
shughuli ya leo tutaihitimisha kwa kuzindua jezi mpya ya timu ya Taifa.
Jezi hizi zitakuwa ni mbili moja ya ugenini na nyingine ya
nyumbani.Tunawapongeza watanzania wote walioshiriki katika kubuni jezi
na mwisho tuliunganisha ubunifu tofauti na kupata jezi itakayozinduliwa
leo.
Ubunifu huu tayari
umetafutiwa hati miliki Brela hivyo TFF tutalinda hakii hii kwa
kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote
watakaodiriki kuchapisha na kuuza kwa magendo jezi hizi.Utaratibu
unafanyika kumpata msambaji mmoja halali atakayesambaza jezi hizi nchini
kwa ajili ya wapenzi wa mpira wa miguu.Ukinunua jezi hii utakuwa
umechangia maendeleo ya mpira wa miguu.
TFF inawashukuru na
kuwapongeza sana Tanzania Breweries ltd ambao ndio wazalishaji wa bia ya
Kilimanjaro Lager kwa sapoti wanayoitia kwa timu ya Taifa na
kutuwezesha kubuni na kuzalisha jezi hizi.Tunawashukuru sana.
Ndugu mgeni rasmi
ninaomba nimalizie kwa kuzungumzia kwa kifupi program yetu ya mpira wa
vijana.kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza soka la vijana TFF tumejipanga
vilivyo kwa mpambano wa hatua za awali za kucheza fainali za vijana za
Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2017.
Mechi za ufaulu
zitafanyika kati kati ya mwaka 2016.TFF tayari tumeunda kikosi cha awali
cha vijana chini ya umri wa miaka 15 kujiandaa na michuano hii.Kikosi
hiki kimetokana na michuano ya copa coca cola ya mwaka jana.
Tunapenda tuchukue fursa
hii kumshukuru Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha nchi yetu
ya Tanzania,kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii,kupata
uenyeji wa fainali za Afrika. Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF
limeipatia Tanzania uenyeji wa fainali za Afrika za vijana umri chini ya
miaka 17 mwaka 2019.
Tunaomba Serikali
itushike mkono katika hili ili tuweze kuandaa mashindano mazuri.Lakini
haitakuwa vyema Tanzania kuandaa mashindano mazuri lakini tukatolewa
hatua ya makundi.Siku ya jumapili tarehe 07/juni TFF tutazindua
mashindano ya taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 mjini mwanza.
Wachezaji bora wa
mashindano haya ndio wataunda kikosi cha awali cha Taifa kwa ajili ya
kushiriki fainali za Afrika watoto umri chini ya miaka 17 mwaka 2109.
Tunaomba Serikali pamoja na wadau wote tushirikiane katika kukilea kikosi hiki ili mwaka 2019 tuwe na timu nzuri.
Tunamshukuru Mh Dr
Fennela Mukangara na wizara nzima ya habari vijana utamaduni na michezo
kwa ushirikiano wanaotupatia katika hatua hizi na katika shughuli
nyingine za kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu.
Ndugu mgeni rasmi ninaomba sasa nikukaribishe uhutubie hafla hii na pia utuongoze katika shughuli zitakazofuata.
Ahsate sana
Jamal Malinzi
Dar es salaam
03/juni/2015
No comments:
Post a Comment