Sheria
Ngowi pembeni yake ni Aj Mynah ambae ni Mkurugenzi wa Black Fox Model
Afrika na anaefuata ni Ednda Ndebalema wa Ndibs Makeup wakizungumza na
wanamitindo hao katika mafunzo yaliyoandaliwa na Black Fox katika klabu
ya Paparaz iliyopo Sleep Way Masaki.
Sheria Ngowi akiwafunda somo wanamitindo.
Wakapata nafasi ya kupiga picha.
Wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Na Evance Ng’ingo
WANAMITINDO
wanaochipukia nchini wametakiwa kujitambua pamoja na kuwa na mikakati
ya kujitangaza zaidi ili kupata soko la ndani na nje ya nchi.
Wito
huo ulitolewa jana na Mwanamitindo mahiri wa mavazi nchini Sheria Ngowi
wakati akizungumza na Wanamitindo kutoka kampuni ya Black Fox Model
Africa.
Ngowi
pamoja na mtaalamu wa urembaji Edna Ndibarema wa kampuni ya Ndiba Style
walialikwa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, ya Black Fox Model Africa, Aj
Mynah kuzungumzia fursa zilizopo katika tasnia hiyo.
Ngowi
aliwataka wanamitindo kuichukulia kazi hiyo kuwa ni sawa na kama kazi
nyingine zenye kipato licha ya kuwa kwa hapa nchini ni fani ambayo
inazidi kukua kwa kasi.
Alisema
kuwa akiwa kama mwanamitindo ametembea nchi mbalimbali kuonesha mavazi
na amekutana na wanamitindo mbalimbali wa kimataifa ambao walianza
kufanya kazi hiyo wakiwa kama wanamitindo wa kawaida.
Alisema
kuwa ili wanamitindo wa Tanzania nao kufikia hatua kama hiyo wanatakiwa
kuwa na mikakati mingi ya kujitangaza ambapo aliwataka kutumia zaidi
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kujitangaza.
Alisema
kwa kwa kutumia mitandao kama Twiter, Facebook, Instagram pamoja na
tovuti nyingine mbalimbali kubwa wanamitindo wanaweza kujijengea jina na
kutumiwa na makampuni mbalimbali kutangaza biashara zao.
Aliongeza
kuwa pia wanatakiwa kuwa na kitabu maalumu chenye picha na nakala zao
mbalimbali zinazoelezea kuhusiana na urefu wao, urefu wa kiuno, urefu wa
nywele na mengineo muhimu ili wazitumie kujitangaza kirahisi zaidi
katika mitandao ya kijamii au hata kuwa nayo wenyewe.
”
Kikubwa ni kujua namna ya kujitangaza hasa zaidi kujionesha utoafuti
wako wewe na wanamitindo wengine na kinachotakiwa ni kujitangaza na ili
kufanikisha hilo yapo mambo mengi ya kuzingatiwa ili kutimiza ndoto
hizo” aliongeza mwanamitindo huyo.
Kwa
upande wake Edna Ndibarema aliwataka wanamitindo kuzingatia suala zima
la usafi hasa katika kujiandaa wakati wa shoo, usafi wa mwili pamoja na
kuimarisha haiba ya sura zao.
Alisema
kuwa wanamitindo wengi wanashindwa kujitambua thamani yao na kujikuta
wakitumiwa vibaya na watu mbalimbali kwa matamanio ya mwili na mengineo.
No comments:
Post a Comment