Pages

Wednesday, June 24, 2015

ROBERTO FIRMINO ASAINI LIVERPOOL KWA DAU LA PAUNI MILIONI 29

Liverpool imefikia makubaliano ya kumsaini Roberto Firmino kwa Dau la Pauni Milioni 29 ambalo litamfanya awe Mchezaji wa Pili kununuliwa na Klabu hiyo kwa Fedha nyingi.
Firmino, mwenye Miaka 23, ni Straika wa Klabu ya Bundesliga huko Germany, Hoffenheim, na sasa yuko Nchini Chile akiichezea Brazil kwenye Fainali za Copa America.
Mkuu wa Liverpool, Ian Ayre, yupo Nchini Chile kusimamia Dili hii ambayo itampa Staa huyo Mkataba wa Miaka Mitano huku tayari inasemekana washaafikiana kuhusu maslahi yake binafsi.
Firmino ameifungia Hoffenheim Bao 49 katika Mechi 153 na Juzi aliipigia Brazil Bao la Pili wakati wanaichapa Venezuela 2-1 na kutinga Robo Fainali ya Copa America.

Mwaka 2011, Liverpool ilimsaini Straika wa Newcastle, Andy Carrol, kwa Dau la Pauni Milioni 35 ambalo ndio kubwa katika historia ya Klabu hiyo.
Hivi karibuni Liverpool ilimnunua Straika wa Burnley Danny Ings pamoja na Kipa Adam Bogdan, Beki Joe Gomez na Kiungo James Milner tayari kwa ajili ya Msimu mpya.
Lakini wapo njiani kumpoteza Staa wao mkubwa Raheem Sterling ambae amegoma kusaini Mkataba mpya na kutaka kuhama huku Manchester City wakitoa Ofa mbili ambazo zimekataliwa.
Roberto Firmino

No comments:

Post a Comment