Pages

Wednesday, June 24, 2015

BUSUNGU AIONGOZA YANGA KUIFUNGA FRIENDS RANGERS LEO



 
Mchezaji wa Yanga Juma Abdul (kulia0 akimtoka mchezaji wa Friends Rangers leo kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Karume


TIMU ya Yanga yenye maskani yake mtaa wa Jangwani na Twiga jana iliifunga Friends Rangers mabao 3-2 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Yanga ambayo ilikuwa inawajaribu wachezaji wake ambao wamesajiliwa msimu huu ilianza kupata bao la kwanza dakika ya 11 lililofungwa na Kpah Sherman akimalizia pasi ya Busungu
Hata hivyo Friends Rangers walisawazisha bao hilo dakika ya 25 lililofungwa na Mussa Juma lakini dakika ya 37 Yanga waliongeza bao la pili lililofungwa na Busungu baada ya kupokea pasi toka kwa Sherman bao lililodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadilikoambapo Yanga iliwatoa Kpah Sherman, Geofrey Mwashaiya, Andre Countinho na kipa Benedicto Tinoco na kuwaingiza kipa Ally Mustapha ‘Barthez’, Amis Tambwe, Simon Msuva na Deus Kaseke.
Mabadiliko hayo yaliongeza mashambulizi kwani kila mchezaji alijitahidi kuwafurahisha mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo lakini mchezaji Cosmas Lewis wa Friends Rangers aliwanyamazisha mashabiki baada ya kusawazisha bao dakika ya 83 kabla ya Busungu kuifungia Yanga bao la ushindi dakika ya 88. 
Friends Rangers ambao wanacheza ligi daraja la kwanza tena bado hawajaanza mazoezi walionyesha kandanda safi mbele ya Yanga ambayo imeanza mazoezi takribani wiki mbili sasa huku ikiwa na wachezaji wake wa kigeni.

No comments:

Post a Comment