Pages

Monday, June 1, 2015

RAFAEL BENITEZ NJIA NYEUPE KUTUA REAL MADRID, MAKAMU WA REAL AWEKA WAZI


Makamu Rais wa Real Madrid ameropoka na kutamka kuwa Rafael Benitez ndie Kocha Mkuu wao mpya.
Benitez anatarajiwa kuachia ngazi kwenye Klabu yake ya sasa Napoli ya Italy mara baada ya kumaliza Mechi yao ya mwisho ya Msimu wa Serie A Leo hii Jumapili.
Lakini, Makamu Rais wa FIFA, Eduardo Fernandez de Bla, akiongea kwenye Kikao cha Mashabiki wa Real hapo Jana, alisema: " Carlo Ancelotti Kocha Bora Duniani kama alivyokuwa Jose Mourinho Miaka Miwili iliyopita na kuanzia Wiki hii, Benitez ndie atakuwa Kocha Bora! "
Wiki iliyopita Real ilimtimua Ancelotti baada ya Msimu huu kutwaa Taji moja tu, Kombe la Klabu Bingwa Duniani, wakati Msimu uliopita walibeba Kombe la Klabu Bingwa Ulaya na Copa del Rey.
Nae Mourinho, ambae sasa ni Bosi wa Chelsea, alifukuzwa na Real 2013 baada ya kutwaa Ubingwa wa La Liga na Copa del Rey, mara moja moja, katika himaya yake ya Miaka Mitatu.
Benitez, Raia wa Spain mwenye Miaka 55, aliiongoza Liverpool kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI Mwaka 2005 na kutwaa EUROPA LIGI na Chelsea Mwaka 2013 na kisha kujiunga na Klabu ya Italy, Napoli, ambayo alitwaa nayo Coppa Italia Mwaka 2014.
Kocha huyo pia aliweza kutwaa Ubingwa wa La Liga mara 2 na UEFA CUP mara moja wakati akiwa na Valencia kati ya Mwaka 2001 na 2004.
Kati ya Mwaka 1993 na 1995 alifundisha Kikosi cha Akiba cha Real Madrid.Rafael Benitez

No comments:

Post a Comment