Pages

Saturday, June 20, 2015

MARIO MANDZUKIC KUTUA JUVENTUS, CARLOS TEVEZ NJIA NYEUPE KUONDOKA

www.bukobasports.comCarlos Tevez Siku zote amekuwa akisisitiza kuwa anataka kumalizia Soka lake kule alikoanzia Utotoni kwenye Klabu ya Nchini kwao Argentina Boca Juniors na ndoto hii sasa iko mbioni kukamilika.
Meneja Mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta, ametoboa kuwa wao washamtambua Straika kutoka Croatia, Mario Mandzukic, ndie atakaembadili Tevez hapo Juve.
Nayo Klabu ya Mandzukic, Atletico Madrid, kupitia Kocha wao Diego Simeone, imedokeza kuwa Straika huyo anaweza kuondoka licha ya wao kumtegemea sana.
Marotta, akiongea na Tuttosport, amesema kuwa wao wanaitambua ndoto ya Tevez ya kurudi kwao Argentina na wanaiheshimu.Pia Meneja Mkuu huyo amesema: "Tunatambua mchango mkubwa wa Tevez kwetu lakini sasa tunangoja majibu na tutajua katika Siku mbili tatu."
Tevez alijiunga na Juve Mwaka 2013 akitokea Manchester City na kuifungia Bao 39 katika Mechi 66.

MARIO MANDZUKIC KUTUA JUVENTUS

No comments:

Post a Comment