Pages

Monday, June 1, 2015

KOMBE LA 2010 AFRIKA KUSINI LILIPIWA

 Waafrika Kusini wakishangilia kombe la dunia mwaka 2010
Magazeti ya Afrika Kusini yanaripoti kuwa nchi hiyo ililipa dola milioni 10 kwa shirika la kandanda linaloongozwa na Jack Warner - mmoja kati ya maafisa wa FIFA wanaotajwa katika tuhuma za rushwa.
Maafisa wa mashtaka wa Marekani wanasema malipo hayo hayakuwa halali - na yalisaidia ombi la Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la mwaka wa 2010.
Lakini rais wa jumuia ya kandanda ya Afrika Kusini, Danny Jordaan, amekanusha hayo.
Maafisa ambao hawakutajwa majina, wanasema fedha hizo zilikusudiwa kuendeleza kandanda kati ya Waafrika wanaoishi uhamishoni.
Na BBC imekuja kujua kuwa mabenki mawili ya Uingereza yanachunguza matawi yake kuhusu fedha katika mabenki hayo za maafisa wa FIFA.
Barclays na Standard Chartered zilitajwa juma lilopita katika mashtaka ya shirika la kuchunguza uhalifu la Marekani, FBI, dhidi ya maafisa wa Shirikisho la Kandandana Duniani.
Benki ya HSBC piya imetajwa.
Babenki hayo hayakutuhumiwa kuwa yalifanya makosa.
Standard Chartered ilisema inajua kuwa malipo mawili ya fedha yaliyopitishwa katika benki hiyo yametajwa, na benki imesema inachunguza hayo.
Barclays na HSBC zimekataa kusema kitu.

No comments:

Post a Comment