Pages

Tuesday, June 9, 2015

Hukumu ya kifo ya watu 11 itadumu Misri

Hukumu ya kifo ya watu 11 itadumu Misri
Mahakama nchini Misri umeamuru kuwa hukumu wa kifo dhidi ya watu 11 waliopatikana na hatia ya kuzua ghasia mbaya wakati wa mechi ya kandanda miaka mitatu iliyopita itadumu.
Kesi hiyo ilihusu ghasia kati ya mashabiki hasimu katika kile kiliitwa kuwa mauaji ya halaiki ya uwanja wa Port Said ambapo zaidi ya watu 70 waliuawa.
 
Ghasia kati ya mashabiki
Maafisa kadha wa polisi walifikishwa mahakamani katika kesi hiyo, lakini hakuna hata moja kati yao aliyehukumiwa kifo. Aliyekuwa mkuu wa usalama katika mji wa Port Said alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.
Polisi walilaumiwa kwa kuwaruhusu mashabiki kutoka timu wenyeji ya al-Masry kuwashambulia mashabiki wa klabu kutoka mjini cairo ya Al-Ahly

No comments:

Post a Comment